Tuesday, December 16, 2008

MIUJIZA YAZIDI KULIPUKA WRM

Wakazi wa jiji la Dar es Salaam na nje ya jiji hilo wanaohudhuria katika huduma ya maombezi ya The Word of Reconciliation Ministries (WRM) lililochini ya Mchungaji Nicolaus Suguye wamezidi kupokea miujiza yao kutoka kwa Mungu baada ya kusumbuliwa na maradhi kwa miaka mingi bila kupona.(Kulia Mchungaji Suguye akiingia katika Huduma ya The Word of Reconcilion Ministries)

Katika hali ya kushangaza watu wengi Eliza Mwita binti aliyezaliwa akiwa kipofu aliombewa katika huduma hiyo na kunza kuona kama kawaidi, huku bibi Sisilia Biti Gulasa ambaye hakuweza kuitambua miaka yake kutokana na uzee, aliponywa ugonjwa wa moyo uliokuwa unamsumbua kwa miaka mitano huku akimaliza kila aina ya tiba bila mafanikio.
Bibi huyo alisema usiku alikuwa halali kutokana na maumivi makali aliyokuwa akiyapata, na alipoenda hospitali kupima alibainika ana moyo alipewa dawa za kila aina lakini haikusaidia mpaka alipoamua kusalimisha maisha yake kwa Yesu ( kuokoka) ndipo alipokea mjiza wa uponyaji.
Alisema kabla ya uponyaji huo alitumia gharama kubwa ya kutaka kuokoa maisha yake kutokana na maumivu makali yaliyokuwa yanamsumbua na kupelekea asipate usingizi nyakati za usiku, lakini baada ya uponyaji huo maumivu hayo hayakumbuki tena na anapata usingizi
safi.
Mbali na hao watu wengine ambao Mungu aliamua kuwaponya na kujitukuza kupitia kwa Mtumishi wake Suguye ni Jastine Mahoka ambaye alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa kansa ya mguu kwa muda mrefu na kupelekea ashindwe kutembea kutokana na mguu huo kuoza na kutoa harufu kali, alijikuta anatembea kama kawaida baada
ya kufanyiwa maombi katika huduma hiyo iliyopo Matembele ya Kwanza Kivule nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam. (kushoto Mchungaji Suguye akimwombea Eliza aliyekuwa kipofu baada ya kufikishwa katika huduma ya Maombezi)
Naye baba mmoja aliyejulikana kwa jina moja, alijikuta anapona vidonda vya tumbo ambavyo vilikuwa vinamsumbua kila nyakati za usiku, na kutumia kila aina ya dawa bila mafanikio huku akipinga uweza wa Mungu
kama anaweza kupona ugonjwa huo.
Akisimuliwa mkasa huo kwa niaba ya mke wake, Maria Sande alisema kuwa mumewe kwa murefu alikuwa anakaidi kwenda katika makanisa ya Kiroho kutokana na kukumbatia dini yake, hata hivyo baada ya kuzidiwa na ugonjwa huo aliomba apelekwe katika huduma hiyo kwenda kuombea baada ya kusikia kuwa watu wengi wenye magonjwa yaliyoshindikana kibinadamu wanaponywa kwa uwezo wa Mungu.
Suguye alisema kuwa watu wengi wamekuwa wakibeza miujiza inayotendeka katika huduma zinazotolewa na watumishi waliopakwa mafuta na Mungu, na kujikuta wanakimbilia kwa waganga wa kienyeji hali ambayo huwasababishia kupoteza fedha nyingi kwa kuwapa waganga hao huku wakikimbia huduma inayotolewa bure na Mungu.
Katika hatua nyingine Mchungaji Suguye alisema kuwa huduma yake ya The Word of Reconciliation Ministries (WRM), inatarajia kufungua chuo cha watumishi wa Mungu kitakachojulikana kwa jina la The Reconciliatio Pastors & Prophets College.
Chuo hicho kinatarajiwa kuanza Januari 1 mwakani kikiwahusisha watu wote wenye wito na kazi ya Mungu watakaomtumikia bila kubagua dini ama dhehebu lolote kwa lengo la kuwa kulitangaza vema neno la Mungu kila pembe ya nchi na dunia kwa ujumla. Hata hivyo tayari nafasi hizo zimeshajaa kwa sasa na kwa watakaotaka kujiunga na chuo hicho waombe nafasi hiyo mwezi April 2009.


Ratiba
Jumamosi saa 9:00 mchana mpaka 12:00 jioni maombezi
Jumapili kuna ibaada mbili
1.Saa
2:00 asubuhi mpaka 7:00

2. Saa 10:00 – 12:00

Jinsi ya kufika katika huduma hiyo, panda magari mpaka Banana, kisha panda magari ya kwenda Kivule, shuka Bustani ya Edeni zamani Matembele ya kwanza Kivule kisha uliza Huduma ya Neno la Upatanisho (The Word of Reconciliation Ministries) watakuelekeza. Wote mnakaribishwa kwa ajili ya uponyaji na matatizo mbalimbali yaliyoshindikana. Ama piga simu no. 0784 448117 au 0715 448117.

1 comment:

13china said...

http://13sex.blogspot.com