Tuesday, December 16, 2008

TUSITOZE FEDHA KWA AJILI YA SEMINA ZA NDOA

Watumishi wa Mungu nchini wametakiwa kuacha kasumba ya kuwatoza fedha waumini wao kwa ajili ya kuwafundisha masomo ya ndoa ili kuziponya ndoa zao.

Kauli hiyo imetolewa na Mchungaji Nicolaus Suguye wa Huduma ya Maombezi ya The Word of Reconciliation Ministries lililopo Kivule Bustani ya Edeni zamani 'Matembele ya Kwanza' nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam, aliyesema kuwa kufanya hivyo ni kushindwa kuwatendea haki wanandoa walio na kipato cha chini.Mchungaji Nicolaus Suguye wa Huduma ya maombezi, The Word of Reconciliation Ministries akifundisha somo la ndoa.
Mchungaji Suguye alisema kitendo cha kuwatofa fedha wanandoa hao kunasababisha wanandoa wengi hasa wenye kipato cha chini kushindwa kuhudhuria katika semina hizo, nakujikuta wakiendelea kuishi maisha ya shida katika ndoa zao.
“ Si jambo la busara kuwatoza fedha wanandoa kwa ajili ya kuendesha semina za somo hilo, k
wa sababu kufanya hivyo kunasababisha somo hilo muhimu walipate watu wenye uwezo kifedha pekee na kujikuta wasiokuwa na pesa wanashindwa kuhudhuria katika semina hiyo kutokana na kipato chao kutoruhusu na hali hiyo imekuwa ikiendelea kuwafanya familia zisizo na fedha kuendelea kuishi maisha ya shida,” alisema Suguye. (Chini Mama Mchungaji akiimba wimbo wa kuabudu baada ya somo la semina ya ndoa)
Katika hatua nyingine Mchungaji Suguye aliwataka watumishi hao kuwa na utaratibu wa kuwafundisha somo la ndoa waumini wao ili kujenga kanisa lililotakatifu kuliko ilivyo kwa maadhi ya makanisa ambayo yamepoa kiroho kutokana na familia nyingi kuwa katika migogoro ya ndoa.
Alisema kanisa lilikiwa na familia ambazo ndoa zake hazina matatizo, Roho wa Mungu hushuka katika ibada na kuhudumia watu wenye shida ikiwa ni pamoja na kuwaponya wenye magonjwa yaliyoshindikana, kwa sababu kila aliyeingia ndani ya kanisa
hilo moyo wake unakuwa na furaha toka nyumbani kwake.
Aidha Mchungaji Suguye alisema siku zote ibada huanzia nyumbani, ambapo wanandoa wanapotoka nyumbani kwao wakiwa wenye furaha, hata kanisani furaha hiyo huongezeka na kujikuta wanamwabudu Mungu katika Roho na kweli na kuifanya ibada hiyo iwe moto.
Alisema familia ikiwa na ndoa yenye amani, chemchem ya mafanikio huonekana hali ambayo husababisha kanisa kukua kiuchumi kutokana na waumini wake kuwa na uwezo kimaisha na kuwa wepesi katika suala la utoaji wa sadaka na fungu la kumi.

No comments: